Majukumu ya CBT

Majukumu ya CBT ni kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Korosho Na. 18 ya mwaka 2009 kama ifuatavyo:

Kushauri Serikali kuhusu sera na mikakati ya maendeleo ya sekta ya korosho.
Kukuza maendeleo ya uzalishaji, usindikaji na masoko ya korosho.
Kusaidia moja kwa moja au kupitia msaada wa kifedha tafiti na maendeleo ya sekta ya korosho.
Kudhibiti na kusimamia ubora wa korosho.
Kukusanya, kuchambua, kuhifadhi, kutumia na kusambaza taarifa au takwimu kuhusu sekta ya korosho.
Kuhakikisha usimamizi sahihi wa Mfuko wa Maendeleo ya Korosho ulioanzishwa chini ya Sheria ya CBT Na. 18 ya mwaka 2009.
Kukuza na kurahisisha uundwaji wa vyama au taasisi zinazohusiana na sekta ya korosho na kuratibu shughuli zake.
Kutunga na kusimamia kanuni za korosho.
Kutoa huduma za ushauri na kitaalamu kwa wakulima wa korosho, wasindikaji, wanunuzi au wauzaji nje.
Kuwakilisha Serikali katika majukwaa ya kimataifa.
Kutekeleza majukumu mengine yanayohusiana na maboresho ya sekta ya korosho kadri uhitaji unavyojitokeza, kama vile:
Kusajili au kutoa leseni kwa wakulima wa korosho, wanunuzi, wauzaji, wasindikaji na wauzaji wa nje.
Kutoa leseni na vibali vya ununuzi na usafirishaji wa korosho nje ya nchi. Kuteua wakaguzi kwa ajili ya ukaguzi wa mashamba ya korosho, viwanda vya usindikaji, maghala na maeneo mengine kwa utekelezaji bora wa masharti ya Sheria ya Sekta ya Korosho ya mwaka 2003.