Kuhusu Bodi ya Korosho Tanzania
Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) ni chombo cha ushirika kilichoanzishwa kwa Sheria Sura ya 203 RE 2023. Imekabidhiwa jukumu la kusimamia maendeleo ya Sekta ya Korosho nchini Tanzania katika kutekeleza majukumu yake. Bodi ya Korosho inatilia mkazo zaidi katika kuboresha obora na ufanisi katika sekta ndogo ya korosho ili kukidhi matakwa ya wadau mbalimbali na hivyo kuwawezesha kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
Dira Yetu
Kuwa taasisi ya udhibiti yenye uwezo na ufanisi kwa ajili ya sekta ya korosho iliyo hai na endelevu.
Dhima Yetu
Kukuza, kusimamia na kudhibiti masuala yote katika sekta ya korosho kwa ufanisi, kwa tija, na kwa haki.
Maadili ya Msingi
Uadilifu
Tunazingatia uwazi, ukweli na uaminifu katika utoaji wa huduma zetu zote kwa umma na wadau wa korosho.
Weledi
Tunatumia ujuzi, maarifa, na viwango vya juu vya kiutendaji katika kutekeleza majukumu yetu ya kila siku.
Ubunifu
Tunahamasisha matumizi ya teknolojia mpya na njia bora za kisasa kutatua changamoto za tasnia ya korosho.
Ushirikiano
Tunathamini mchango wa kila mdau na kufanya kazi kwa umoja ili kufikia malengo yetu ya pamoja.
Uwajibikaji
Tunawajibika kwa maamuzi na matendo yetu, tukihakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi na tija kwa maendeleo ya kilimo.